Nachukua Nafasi hii kukukaribisha wewe unaesoma post hii wakati huu. Kwanza nakushukuru kwa kunipa muda wako wa thamani sana na nakuhakikishia kwamba lazima upate kitu katika shule hii huru uliyozuru hii Leo.
Kwa ufupi sana, Blog yetu inaitwa PLATO ACADEMY.
Lengo kuu LA blog hii ni kukupa maarifa sahihi na ya msingi katika maisha yako. Tunapenda kuona wasomaji wetu wakifanikiwa katika nyanja mbalimbali za maisha yao kama vile KAZI, BIASHARA, UJASIRIAMALI, ELIMU, MAHUSIANO, NDOA, UONGOZI n.k
PLATO ACADEMY haitaishia hapo tu, pia itatoa fursa kwa wanafunz kujipatia NOTES, PAST PAPERS, PAMPHLETS, na MATILIO ya masomo mbalimbali kuanzia elimu ya msingi mpaka chuo. Na kwa watu wazima tutakuwa na lumbesa LA vitabu vitakavyokupa maarifa yatakayokuongoza kutimiza malengo yako. Nia yetu ni kuona wasomaji wetu wa rika zote wanafanikiwa na kwakuwa Elimu ni moja kati ya funguo muhimu za mafanikio. HATUTAIACHA NYUMA KAMWE!
MICHEZO na BURUDANI pia ni sehemu ya vyakula vitamu vitakavyoandaliwa hapa PLATO ACADEMY ili kuimarifa Afya ya mwili na akili kwa wasomaji wetu.
Napenda kukukaribisha tena na tena ewe msomaji wetu.
Jina language ni JOHN JONAS KIWOVELE. mwanzilishi na msimamizi mkuu wa hii blog.
Mawasiliano yangu: +255 766 848616
Ahsante sana.
Comments
Post a Comment